Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo Asema nchi na mipaka yake iko salama, na itaendelea kuwa salama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amesema mchango mkubwa uliotolewa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama utaendelea kuwa alama isiyofutika.

Amesema katika uhai wake Dkt Magufuli alivipenda vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na aliviwezesha ili viweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Akitoa salamu za vyombo vya Ulinzi na Usalama katika uwanja wa Magufuli wilayani Chato mkoani Geita inapofanyika Misa Takatifu ya Mazishi ya Dkt Magufuli, Jenerali Mabeyo amesema  Dkt Magufuli alivishirikisha vyombo hivyo katika miradi mikubwa ya kiuchumi akimini kuwa vita ya kiuchumi ni ngumu tofauti na  vita nyingine yoyote.

Amemuhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa, vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama nchini vitaendelea na jukumu la kuwalinda Watanzania na mali zao pamoja na Rasilimali zote za Taifa.

Pia amewahakikishia Watanzania  kuwa nchi na mipaka yake iko salama, na itaendelea kuwa salama.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad