Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Mmiliki hoteli ya Snowcrest kuzikwa Jumatatu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREArusha. Mmiliki wa hoteli ya Snowcrest ya jijini Arusha, William Mollel atazikwa Jumatatu Machi 15, 2021 wilayani Arumeru mkoani humo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi Machi 13, 2021 ndugu wa mfanyabiashara huyo, Lemburis  Sirikwa amesema kwa sasa wanaendelea na taratibu za mazishi.

Mmoja wa marafiki wa mfanyabiashara huyo,  John Laizer amesema Mollel licha ya kumiliki Snowcrest  pia alikuwa anamiliki hoteli nyingine eneo la Moivaro, kujishughulisha na kilimo na ufugaji.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa viwanda na kilimo (TCCIA) Mkoa wa Arusha,  Walter Maeda amesema, “alikuwa mfanyabiashara mzuri na mkulima,  mjomba wake ndiye mwenyekiti wa chama cha wakulima(TFA).”


 
Mollel  alinunua hoteli hiyo mwaka 2014 kutoka kwa mfanyabiashara  Wilfred Tarimo na mara ya mwisho kuzungumza na Mwananchi alisema aliinunua kwa mkopo na kutaka kuigeuza kuwa ya kimataifa.

Post a Comment

0 Comments