Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mshindo Msola: Sikumpigia Metacha Mnata na kumtuhumu ila simu yangu ilidukuliwa

  MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msola amesema kuwa namba yake walihack, 'dukua' jambo lililofanya aonekane amempigia mchezaji wa timu hiyo Metacha Mnata. 

Kipa Mnata ambaye alikuwa langoni Machi 7, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati ubao ukisoma Polisi Tanzania 1-1 Yanga aliokota nyavuni mpira wa Pius Buswita dakika ya 89.


Machi 8 aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwaaga mashabiki pamoja na viongozi kisha ujumbe huo aliufuta ambapo inaelezwa kuwa alipokea ujumbe kutoka kwa Msola akimpa mzigo wa lawama.


Msola amesema kuwa hana tabia ya kuzungumza na wachezaji zaidi akiwafuata kambini huwa anatumia muda huo kuzungumza nao kwa pamoja na sio mchezaji mmoja na hana Utamaduni huo.


"Nilitumiwa taarifa ya kwanza niliitazama ila sikuelewa mpaka nilipotumiwa maelekezo na mtu mwingine kwamba inaelezwa nimenpigia simu Metacha jambo ambalo sio kweli.


"Meneja wa Metacha, Jemedar Said aliniambia na kunionyesha namba yangu, nilishangaa na kujua kwamba hii ni vita maana kama mpaka mtu anatumia namba yako kumpigia mtu sio sawa.


"Nina uhakika namba yangu walihack hata kama tukienda Tcra itaonyesha kwamba sikuwa mimi ambaye nilimpigia hiyo simu,".

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments