Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mume wa Malkia Elizabeth ahamishwa hospitali

Mume wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, Mwanamfalme Phillip amehamishiwa katika hositali nyingine mjini London kwa matibabu zaidi baada ya kupata maambukizo. 


Kwa mujibu wa Kasri la Malkia, Mwanamfalme Phillip aliondoka kwenye hospitali binafsi ya Mfalme Edward wa Saba mjini London ambako alikuwa amelazwa kwa takriban wiki mbili kwenda katika hospitali ya Mtakatifu Bartholomeo kufanyiwa vipimo vya moyo na matibabu mengine. Madaktari wa hospitali hiyo wataendelea kumtibu maambukizi aliyoyapata, pamoja na kufanyiwa vipimo vya moyo. Taarifa ya Kasri imesema mume huyo wa Malkia Elizabeth yuko sawa na ataendelea kupatiwa matibabu na anatarajiwa kubakia hospitali hadi mwishoni mwa juma hili.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments