Mwambusi Akabidhiwa Yanga Mazima

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA






IMEELEZWA kuwa Juma Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga atakiongoza kikosi hicho kwenye mechi zote ambazo zimebaki ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

 

 

Mwambusi alirejeshwa kazini mara baada ya Cedric Kaze ambaye alikuwa Kocha Mkuu pamoja na Nizar Khalfan ambaye alikuwa msaidizi wake kufutwa kazi Machi 7 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu.

 

 

 

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa sababu za kulifuta benchi la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kaze ni matokeo mabaya.

 

 

 

“Ikiwa ni timu inapata matokeo mabaya hapo ni lazima sababu itafutwe na baada ya kutafuta sababu ikaonekana kwamba makosa yapo kwenye benchi la ufundi.

 

 

 

“Hivyo tukakubaliana kwamba ni lazima benchi lifutwe. Kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kumsaka kocha mpya ambaye atakuja hivi karibuni ndani ya kikosi chetu.

 

 

 

“Zaidi ya CV 72 zimepokelewa na mchujo unafanyika ili kupata kocha ambaye atakidhi vigezo kabla ya kumtangaza na tunaamini kwamba atakuwa kocha mzuri hivyo mashabiki wasiwe na mashaka,” amesema.

 

 

 

Habari zimeeleza kuwa Yanga imekubaliana na Mwambusi ambaye alijiweka kando kwa muda ndani ya kikosi hicho kutokana na matatizo ya kiafya kusimamia kikosi hicho mpaka msimu wa 2020/21 utakapokamilika.

 

 

 

Kwa sasa Yanga nafasi ya kwanza na ina pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23 ndani ya Ligi Kuu Bara.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad