Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mwana Mieleka Randy Orton Akasirishwa na Kauli ya Soulja Boy Kuwa Mchezo wa Mieleka ni Maigizo Matupu

 


Kauli ya Soulja Boy kwamba mchezo wa Mieleka hauna uhalisia (fake) umemkasirisha mwanamieleka wa WWE, Randy Orton. Wawili hao wamejibizana kwenye mtandao wa twitter huku Randy akionesha wazi hasira zake. Kubwa lililomkera The Viper, Apex Predator, The Legend Killer, Randy Orton ni Soulja Boy kuudhihaki mchezo ambao unamfanya apate kipato na aishi vizuri na familia yake.


Soulja Boy anaonekana kama amejipanga kwani alienda mbali zaidi hadi kutaka kuzichapa na Randy kama yupo tayari. Staa mwingine alionekana kukerwa na kauli hiyo ya 'The Crank That' Hit star Soulja Boy, ni T-BAR wa kundi la Retribution.


Hii imekuja kufuatia mapema wiki hii, Soulja Boy kuandika kupitia twitter kwamba game ya Hip Hop kwa sasa imekuwa feki kama ulivyo mchezo wa mieleka chini ya WWE.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments