Naibu Waziri azungumza na Wafungwa “Rais Magufuli anawategemea”

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Serikali imewaasa wafungwa wote nchini kuzidisha kufanya ibada sambamba na kuzidisha kumuomba Mungu ili wakitoka waende kuwa raia wema pamoja na kukamilisha ndoto zao walizokua nazo
Kuli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo katika kikao kikao cha ndani kilichohusisha wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Sindida mjini ambapo pia alipata fursa ya kuwasikiliza wafungwa ambao walitoa maoni,mapendekezo na changamoto mbalimbali walizokua nazo ikiwemo kuchelewa kwa upepelezi wa kesi zao.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawategemea sana hasa vijana na Taifa hili linawategemea sana, hapa naona vijana mko wengi vijana ndio nguvu kazi ya Taifa, sasa endeleeni kuwa raia wema, ukitoka hapa kifungoni nenda kawe raia mwema” Naibu Waziri Chilo

“Mkitoka hapa nendeni mkaendeleze ndoto zenu,fanyeni ibada muombeni mungu sana fanyeni ibada huwezi kujua ukitoka hapa utaenda kuwa nani maana historia inatuonyesha wako watu mbalimbali walikua wafungwa lakini walivyomaliza vifungo vyao walienda kuwa viongozi wakubwa tu” Naibu Waziri Chilo

Akisoma taarifa ya gereza mbele ya Naibu Waziri, Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Singida, amesema katika gereza hilo kuna shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo kilimo cha mahindi,maharage,kilimo cha mbogamboga,ufyatuaji wa tofali,ufugaji wa Samaki,ujenzi wa nyumba za makazi ya askari.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad