Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Namungo FC kuvaana na Pyramids leo

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREHEMED Morocco Seleman, Kocha Mkuu wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa wanahitaji pointi tatu mbele ya Klabu ya Pyramids leo kwenye mchezo wao wa hatua ya makundi.

Namungo inayowakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, leo Machi 17 itakuwa Uwanja wa Mkapa kuikabili Pyramids ambapo ni mchezo wa pili.


Ule wa awali uliochezwa ugenini, Namungo ilipoteza kwa kufungwa bao moja bila dhidi ya Raja Casablanca hivyo leo wanakazi ya kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo.


Kwenye msimamo inakutana na Pyramids ambayo ina pointi tatu baada ya kushinda mbele ya Nkana FC huku Namungo ikiwa haijakusanya pointi kibindoni.


Morocco amesema:-“Tunaiheshimu Pyramids, ni timu kubwa. Tunaenda kuikabili tukiwa na malengo ya kupata alama tatu. Hautakuwa mchezo rahisi ila tuko tayari” .

Post a Comment

0 Comments