"Nisamehe huko ulipo" - Msanii TID

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Ikiwa leo ni siku ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, msanii wa BongoFleva TID amemuomba msamaha Hayati Magufuli kwa kushindwa kufika kwenye msiba wake Wilayani Chato Mkoani Geita.

 

Akiomba msamaha huo kupitia post yake ya mtandao wa Instagram TID ameandika kuwa "Hakika Ijumaa ya leo itabaki kuwa kwenye kichwa changu, maneno peke yake hayatoshi, naomba Allah akusamehe madhambi yako, pia huko ulipo nisamehe kwa kushindwa kufika mazikoni Chato" 


Wasanii wengine waliondika kuhusu siku hii ya mazishi ya Hayati Magufuli ni Dogo Janja na Mwana Fa ambapo post zao zinaeleza kuwa 


"Leo ni siku ngumu sana kwa Taifa letu la Tanzania, wananchi wako tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda zaidi, Allah akupe kauli thabiti pumzika kwa amani baba" Dogo Janja 


"Kifo hakikwepeki, na mwanadamu akitekeleza wajibu wake kwake na kwa watu wake anafikwa na kifo, naamini Mzee wangu John ‘Walwa’ Joseph Magufuli ametekeleza wajibu wake duniani ipasavyo na anakwenda akiwa amemaliza kazi iliyomleta, anakwenda akiwa na amani moyoni mwake" Mbunge wa Jimbo la Muheza, Tanga na msanii Mwana Fa

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad