Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Fiston: Sisi Ndiyo wa Kulaumiwa
MSHAMBULIAJImpya wa Yanga raia wa Burundi, Fiston Abdoul Razak, amekiri kuwa, wao kama wachezaji ndiyo wanapaswa kubeba lawama kutokana na mwenendo mbaya wa kikosi chao katika siku za hivi karibuni.


Yanga imekuwa na mwenendo wa kusuasua katika siku za hivi karibuni ndani ya ligi hiyo ambayo bado wameendelea kuwa vinara wakitofautiana pointi tano na Simba wanaoshika nafasi ya pili.

 

Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Yanga kwenye dirisha dogo msimu huu, tayari amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao mawili katika michezo mitano aliyocheza.

 

Akizungumza baada ya mchezo wa sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania, Jumapili, Fiston alisema: “Kwa upande wangu nadhani sisi wachezaji ndiyo tunapaswa kulaumiwa kutokana na matokeo haya, benchi la ufundi limekuwa likifanya kazi kubwa kutusisitiza juu ya kumaliza mapungufu yetu lakini mara kwa mara tumeshindwa kutekeleza.

 

“Kwa mfano kwenye mchezo huu dhidi ya Polisi tulicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi ambazo hatukuweza kuzitumia, lakini hata baada ya kupata bao moja tulishindwa kuwa na umakini katika kujilinda na kuruhusu wasawazishe dakika za mwisho, ukiangalia vizuri hili ni tatizo linalojirudia na mara zote tumekuwa tukirekebishwa.”

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments