Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Polisi Wamsaka Kigogo wa Twitter Kuzusha Hofu

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam linamsaka mwanaharakati anayejiita jina la Kigogo katika mtandao wa Twitter.

‘Mwanaharakati’ huyo anadaiwa kuzusha hofu baada ya kusambaza taarifa za uongo, kwamba Rais John Magufuli anaumwa.

 

Taarifa hiyo imetolewa na Ramadhani Kingai, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinondoni leo Jumamosi tarehe 13 Machi 2021, wakati akizungumza na vyombo vya habari mkoani Dar es Salaam.

 

Kamanda Kingai amesema, jeshi hilo linaendelea kumfuatilia Kigogo, na kwamba wakati wowote litamkamata kujibu tuhuma zinazomkabili za kumzushia ugonjwa Rais Magufuli.

 

“Bado tunaendelea kufuatilia taarifa za wengine ambao wanasambaza taarifa za kizushi, yeyote atakayesambaza tunapekua kila sehemu, tutazifanyia kazi kuhakikisha wanaohusika wanachukuliwa hatua za kisheria.

 

“Huyu anayeitwa Kigogo ni mhalifu kama wengine, tunaendelea kupekua kuhakikisha na yeye tunamtia mbaroni. Muda, siku haijafahamika ila tutamkamata tu,” ameahidi Kamanda Kingai.

Post a Comment

0 Comments