Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa CCM

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, amesema kuwa Kamati Kuu imeelekeza kuwa ndani ya muda mfupi ujao utaitishwa mkutano mkuu kwa ajili ya kupendekeza jina la atakayekuwa Mwenyekiti wa chama hicho baada ya Dkt. John Magufuli, kufariki dunia.

 


Polepole ametoa kauli hiyo hii leo Machi 20, 2021, wakati akitoa mrejesho juu ya kile ambacho kimejadiliwa na Kamati Kuu iliyoketi leo kwenye ofisi ndogo za chama hcho zilizopo Lumumba Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa, hawana jina jingine zaidi ya jina la Mhe. Samia Suluhu Hassan mbaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


"Kamati Kuu imeelekeza ndani ya muda mfupi kutoka leo, utaitishwa mkutano mkuu maalumu wa CCM ambao utakuwa na agenda moja ya kupendekeza jina moja tu na hatuna jina jingine jina ni la Rais Samia kuwa Mwenyekiti wa CCM," amesema Polepole.


Pia Polepole, amewasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli, "Kamati Kuu imeelekeza na chama kitatekeleza kwamba, wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM hawa ni viongozi wenzake na Hayati Dkt. Magufuli wa kitaifa wenye dhamana ya usimamizi wa jumla wa chama watashiriki shughuli ya maziko kule Chato," ameongeza.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments