Sababu za mwandishi wa BBC Girmay Gebru kukamatwa na jeshi Ethiopia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Girmay Gebru , anayeifanyia kazi idhaa ya BBC Tigrinya alikamatwa pamoja na watu wengine wanne katika mgahawa mmoja katika mji mkuu wa jimbo hilo Mekelle .

Walioshuhudia waliambia BBC kwamba watu watano walikamatwa na wanajeshi waliokuwa wamevalia sare za kijeshi kabla ya gari walimokuwa kusindikizwa na magari mawili ya kijeshi.

Haijulikani ni kwanini watu hao watano walikamatwa . BBC imepokea ripoti kwamba mwanahabari wake alikamatwa na kupelekwa katika kambi moja ya kijeshi mjini Mekelle.

Jimbo la Tigray limekuwa chini ya usimamizi wa jeshi tangu mwezi Novemba , wakati waziri mkuu Abiy Ahmed alipotangaza kwamba majeshi ya serikali yalichukua udhibiti wa eneo hilo kufuatia mashambulizi ya kuwafurusha wapiganaji wa Tigray Peoples Liberation Front TPLF.

Mgogoro huo uliongezeka baada ya wapiganaji wa TPLF kudhibiti kambi moja ya wanajeshi wa serikali katika jimbo la Tigray.

Mamia wameuawa na makumi ya maelfu kuwachwa bila makao katika vita hivyo , na kuna wasiwasi mkubwa kuhusu kuripotiwa kwa ukatili na kuenea kwa mzozo mbaya wa kibinadamu.

Baada ya kuzuiwa kwa vyombo vya habari vya kimataifa kwa mwezi mmoja kuingia katika jimbo hilo, serikali wiki iliopita iliwaruhusu wanahabari wa kimataifa kuripoti kutoka Tigray.

Mwandishi huyo wa BBC alikamatwa siku mbili baada ya waandishi wengine wawili kutoka nchini humo ambao walikuwa wakifanyia kazi vyombo vya habari vya AFP na Financial Times kukamatwa.

Mwandishi mwengine kutoka nchini humo , Tamirat Yemane pia alikamatwa na wanajeshi hao kwa sababu zisizojulikana.

Afisa mmoja wa chama tawala nchini Ethiopia alionya wiki iliopita kwamba serikali itachukua hatua dhidi ya wale wanaopotosha vyombo vya habari vya kimataifa.

AFP na Financial Times vimepokea idhini kutoka kwa Mamlaka ya kurusha matangazo nchini Ethiopia EBA na wizara ya Amani kusafiri hadi Tigray ili kuripoti mzozo huo.

”Hatujaarifiwa kuhusu mashtaka yoyote dhidi ya Fitsum Berhane. Ushirikiano wake na chombo chengine cha habari haufai kuwa sababu ya kukamatwa kwake , na tunatoa wito aachiwe mara moja”, alisema Phil Chetwynd, Mkurugenzi wa habari wa AFP, katika taarifa.

Chombo cha habari cha Financial Times kilisema katika taarifa fupi kwamba kilikuwa ”kinachukua kila hatua” ili kuhakikisha kwamba wakalimani hao wanaachiwa.

Licha ya waziri mkuu Abiy kutangaza ushindi baada ya wanajeshi wa serikali kuukomboa mji mkuu wa jimbo hilo Mekelle mwezi Novemba , ghasia zimeendelea katika eneo hilo huku hali ya hatari ikiwekwa.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad