Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Samia aeleza maneno aliyoambiwa na Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa wakati anataka kuanza ziara yake mkoani Tanga alimtaarifa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, ambapo alimuambia kwamba aendelee tu na ziara yake kwani yeye anaendelea vizuri.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 22, 2021, Jijini Dodoma, wakati akitoa hotuba kwa Watanzania katika shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri.

 

"Nashukuru nilipata fursa ya kuongea naye siku chache kabla ya kifo chake, pale nilipomtaarifu kwamba nakwenda kwenye ziara Tanga naye aliniambia, Samia usiwe na wasiwasi naendelea vizuri nenda kafuatilie utekelezaji wa Ilani ya CCM kama tulivyowaahidi wananchi, wape salamu zangu waambie nawapenda sana," ameeleza Rais Samia."Na hayo ndiyo yalikuwa maneno yake na mimi ya mwisho sikujua kwamba maneno yale yalikuwa ya kuniaga na kuwaaga Watanzania, sikujua kwamba sitapokea simu yake tena zile simu za asubuhi ‘wewe umelala mpaka saa hizi amka’, kuna hili na lile nenda kafanye sikujua kwamba sitashauriana naye tena ni jambo ambalo litanichukua muda kuzoea," ameongeza Rais Samia.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments