Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Sarah Amrusha Roho Harmo, Anunua Ferrari Mpya


SARAH Michelotti, aliyekuwa mke wa staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, amemrusha rohoo laivu jamaa huyo kwa kujinunulia gari la kifahari aina ya Ferrari; siku chache baada ya kumuanika kuwa aliachana naye kwa sababu ya skendo ya usaliti.

Kwa mujibu wa Sarah, kwa sasa anasukuma Ferrari nyeupe huku akirusha vijembe vinavyoaminika kumlenga mpenzi wa sasa wa Harmonize au Harmo, Kajala Masanja;“Kama nilivyosema, siwezi kuacha Ferrari na kutembelea Crown (aina ya gari ambalo Harmo amemnunulia Kajala).

Mbali na hayo, Sarah aliendelea kurusha vijembe kwamba yeye anaendesha gari la jasho lake tofauti na wengine wanaoendesha magari ya kupewa huku akijiita bosi.

Katika mahojiano yake ya mapema wiki hii, Sarah alidai kwamba tayari amefungua madai ya kumdai Harmo talaka tangu mwezi Disemba, mwaka jana.“Harmonize alinidanganya kwamba Kajala ni dada yake,” anasema Sarah.


 
Sarah aliendelea kusema kuwa, yeye na Harmo itabidi wagawane mali walizochuma pamoja kwani atafuata utaratibu wa kisheria.Kwa sasa Harmo yupo kwenye mapenzi mazito na mwigizaji Kajala ambapo kapo yao ndiyo inayotrendi zaidi.
“Nilipoanza uhusiano naye (Harmo) alikuwa anatoka kimapenzi na Jacqueline Wolper, lakini wakati huohuo pia alikuwa anatembea na Kajala kwa sababu nilikuwa ninaona SMS zao.

Sina tatizo na Kajala, lakini nina tatizo na mume wangu kwa sababu alinidanganya,” anasema Sarah ambaye wataalam wa mambo wanasema bado anampenda Harmo.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments