Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Serikali haijatuma Askari kufunga maduka Dar- RC Kunenge

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge, amesema Serikali haijatuma askari kuamuru kufunga maduka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wafanyabiashara kufuatia taharuki iliyozuka kwa kile kilichodaiwa kuwa serikali imetuma askari waamuru maduka yafungwe katika siku ya leo ya maombolezo ya kitaifa ya Hayati Dk. John Magufuli.

Kunenge amesema: "Nikiwa Mkuu wa Mkoa huu serikali haijatoa agizo hilo, Kama kuna mtu anafanya hivyo ni muhuni na tapeli, endeleeni na biashara zenu bila wasiwasi," amesema Kunenge.

Aidha Kamanda wa polisi Kanda ya Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ametangaza watu wawili tayari wanashilikiliwa kufuatia sakata hilo

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments