Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Serikali Kumfanyia Majaribio Mtoto CharlesMTOTO Charles Mathias Mbena (6) mkazi wa Kibungo Juu, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ameonesha kipaji cha hesabu ambapo anaweza kujumlisha na kutoa hesabu za makumi na malaki bila kutumia karatasi.

 

Charles anayesoma Darasa la Awali katika Shule ya Msingi Nyigwa ametakiwa kufanyiwa majaribio ili kumpeleka katika Shule na Darasa analostahili.

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema wamegundua ana kipaji hivyo watamfanyia majaribio.

 

Katika hatua nyingine Katibu Tawala ameelezea azma yao ya kuboresha mazingira ya Shule ya Msingi Nyigwa kwa kuijengea madarasa manne mbali na mawili ambayo yanamaliziwa na Mkurugenzi.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments