Simba Kupata Pointi za Mezani kwa Merrikh, Kisa Kizima Hichi Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




SIMBA huenda ikapata ushindi wa mezani dhidi ya Al Merrikh kutokana na timu hiyo ya Sudan kudaiwa kuwatumia wachezaji wawili ambao hawakupaswa kucheza katika mchezo baina yao uliochezwa jijini Khartoum, Jumamosi iliopita ambao uliisha kwa sare tasa.

Taarifa za uhakika ambazo uongozi wa Simba umedai kuzinasa kutoka Sudan kwa ushahidi wa nyaraka mbalimbali, zimeonyesha kuwa wachezaji hao Ramadan Agab, Mohamed Bakhit Mahmoud Mohamed, walicheza mechi hiyo huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita waliyopewa na Chama cha Soka Sudan (SFA)

Ushahidi wa barua ambao Simba wameupata na kuionyesha Mwanaspoti nakala, unaonyesha kuwa SFA iliwafungia wachezaji hao kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mikataba katika timu mbili tofauti, adhabu ambayo inaishia katikati ya Aprili

"Hii ni nakala ya uamuzi. Kimsingi wachezaji hao wawili walisaini mikataba miwili tofauti na Al Merrikh na Al Hilal na wamefungiwa kucheza kwa muda wa miezi sita.


Barua hii ni ya Katibu Mkuu wa Al Merrikh ambayo walimpa kocha kwamba anaweza kuwatumia wachezaji wawili waliofungiwa. Wachezaji hao hawakucheza mechi yoyote ya Al Merrikh hadi sasa. Wamefungiwa kucheza hadi katikati ya Aprili. Wamefanya uamuzi wao wenyewe," alisema mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

Ikiwa itabainika ni kweli Al Merrikh waliwachezesha wachezaji ambao hawakustahili kucheza, itaondolewa mashindanoni

"Timu itakayomchezesha mchezaji aliyesimamishwa au asiyeruhusiwa itahesabika imepoteza mchezo husika na moja kwa moja itaondolewa mashindanoni ikiwa kamati ya mashindano ya Caf itajiridhisha na hoja zitakazowasilishwa," inasema kanuni ya saba.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad