Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Simba Yaibana Mbavu Al Merrikh Sudan


LICHA ya kupata sare ya bila kufungana dhidi ya Al Merrikh ya Sudan Simba imeendelea kuongoza kwenye msimamo wa kundi A kwa kufikisha alama 7 hivyo kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga robo fainali.

 

Mechi hiyo imechezwa leo jioni Machi 6, kwenye dimba la Al Hilal, Khartom Sudan.

 

Simba imeingia kwenye mechi hiyo wakijilinda kwa kumiliki mpira wakati mwingi wa mchezo licha ya Al Merrikh kupata nafasi kadhaa kipindi cha kwanza wakitumia mpira ya krosi na kona lakini umakini wa washambuliaji wao umewakoseha ushindi.Simba msimu imeweka rekodi baada ya mechi tatu wakiwa hajapoteza mchezo na hawajaruhusu wavu wake kuguswa.

 

Mabingwa hao wa Tanzania wanaongoza msimamo wa kundi A wakiwa na Alama 7 wakifuatiwa na Al Ahly na As Vita wenye alama 3 na Al Merrikh wanaburuza mkia wakiwa na alama 1.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments