Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Stamina Afunguka Kuhusu Mama Mtoto Wake

  


Msanii wan HipHop Stamina Shorwebwenzi amei-dedicate siku hii ya wanawake duniani kwenda kwa mama wa mtoto wake kwa kusema ni mpambanaji pia alikuwa anakaa getini kukusanya pesa wakati anafanya show mikoani.

 

Akizungumzia hilo kwenye kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio, Stamina amesema alishangazwa na kitendo hicho kwani hakutegemea kama mpenzi wake huyo atafanya jambo hilo kwa zaidi ya mikoa 15.


"Ukiachana na mama mzazi siku ya wanawake duniani naipeleka kwa Mama Lionel, kipindi nakutana naye sikutegemea kama ni mpambanaji alinishangaza kwani nilikuwa na ziara zangu za chaka kwa chaka za mikoani akasema twende wote, yeye alikuwa anakaa getini kuchua pesa wakati nafanya show kwenye jukwaa na alikuwa anawakazia kinoma noma" ameeleza Stamina

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments