Ticker

6/recent/ticker-posts
.

TAKUKURU wamsaidia mwalimu aliyechanganyikiwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


TAKUKURU mkoa wa Katavi imefanikiwa kumrejeshea kiasi cha shilingi milioni 20, Mwalimu mstaafu George Kanyukamalunde, ambaye ameugua ugonjwa wa kuchanganyikiwa mara baada ya kudhulumiwa pesa zake na mtu ambaye alimkopa kiasi cha shilingi milioni 10 baada ya mafao yake kuchelewa.

 

Wakizungumza mara baada ya pesa hizo kukabidhiwa mtoto wa Mwalimu huyo anayeitwa Genuine Kanyukamalunde, pamoja na mke wa mwalimu huyo wamesema kuwa fedha hizo zitamwezesha kuendelea kupata matibabu mara baada ya kupata matatizo hayo.


Kwa upande wake mwalimu huyo mstaafu alipopewa nafasi ya kuishukuru TAKUKURU kwa kumrejeshea pesa zake lakini kutokana na hali yake ya kiafya, alishindwa kuzungumza chochote na badala yake aliangua kilio kwa uchungu.


Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Christopher Nakua, amesema mkopeshaji huyo alichukua kiasi cha shilingi milioni 25 kutoka kwa mwalimu huyo na alifanikiwa kuzichukua kwa sababu kadi ya benki na namba ya siri alikuwa nayo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments