Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Trump Aibuka Upya, Atoa Kauli Hii

ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amezungumza kwa mara ya kwanza tangu Joe Biden kuwa Rais wa nchi hiyo, na kusema kuwa hana mpango wa kuanzisha chama kipya cha siasa na badala yake ameahidi kuwa ataendelea kuungana na wana Republican.

 

 

Akizungumza akiwa Florida jana katika hotuba yake kupitia mkutano wa ‘Conservative Political Action Conference’ (CPAC), Trump amesema kitendo cha kuanzisha Chama kipya kitagawanya kura za Republican na kupelekea chama hicho kisishinde tena.

 

 

Trump ambaye aliondoka madarakani mwezi uliopita, Januari 20, 2021, amemkosoa Rais Biden kwa kubadili yaliyofanywa katika Utawala wake ikiwemo masuala ya Uhamiaji na Usalama katika mipaka.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments