Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Ujumbe mzito wa Harmonize kwa watoto wa kike


Kuelekea siku ya wanawake duniani, msanii Harmonize ametoa wosia kwa watoto wote wa kike ambapo amewaambia  wawe na maamuzi sahihi kwa wanachotaka kufanya kwenye maisha kwa sababu hakuna kitu kipya kwenye dunia.


Akizungumzia hilo kupitia kamera ya EATV & EA Radio Digital, Harmonize amesema akiona mtoto wa kike anakosea basi anahisi kama mwanae Zulekha ndiyo kakosea hivyo amewaomba wafanye vitu kwa wakati sahihi."Mtoto wa kike yeyote ambaye ananitazama sasa hivi anatakiwa ajue kwamba yeye ndio ana maamuzi ya kuchagua kutaka kuwa nani lakini hakuna kitu kipya kwenye hii dunia bibi yako, mama, dada na shangazi vyote walishafanya hivyo ni bora kuwa makini na kufanya vitu kwa wakati sahihi" amesema Harmonize

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments