Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Urusi yamrejesha nyumbani balozi wake Marekani
Urusi imemuita balozi wake nchini Marekani Anatoly Antonov kwa mashauriano mjini Moscow baada ya rais wa Marekani Joe Biden kusema rais wa Urusi Vladimir Putin atalipa kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.Biden alitoa kauli hiyo jana Jumatano baada ya ripoti ya shirika la kijasusi la Marekani kuunga mkono madai ya muda mrefu kwamba rais Putin alihusika kuongoza juhudi za Urusi kuuingilia uchaguzi wa Marekani, madai ambayo Urusi yenyewe imeyapuuza ikisema hayana msingi wowote.

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Urusi imesema katika taarifa kwamba imemuita balozi Antonov kujadili mustakhabali wa mahusiano baina ya Urusi na Marekani.

Hatua hiyo inanuiwa kuhakikisha mashirikiano kati ya nchi hizo mbili hayavurugiki zaidi kwa kuzingatia athari zinazoweza kujitokeza.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments