Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Video ya wanafunzi waliotekwa yaibuka Nigeria

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Wanafunzi waliotekwa nyara katika jimbo la Kaduna kaskazini magharibi mwa Nigeria siku mbili zilizopita wameonyeshwa katika mkanda wa video unaoitisha fidia katika kituo cha televisheni nchini humo usiku wa kuamkia leo. 

Video hiyo imeonyesha picha za kutisha ikiwa ni pamoja na wasichana hao wakipiga kelele wakati wanachapwa na watekaji huku picha nyengine ikionyesha wasichana wengine wakiwa wameketi sakafuni wakiwa nusu uchi. 

Alhamisi wiki hii, watu wenye silaha waliwateka nyara wanafunzi 39, kati yao wasichana 23 na wavulana 16 wa Chuo cha Shirikisho cha Masuala ya Misitu katika jimbo la Kaduna. Aidha picha nyengine za video hiyo zimemuonyesha mwanamume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Benson Emmanuel akiiomba serikali kuwasaidia, lakini ameonya kuwa juhudi za kuwaokoa zitaweka maisha yao katika hatari. 

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa wazazi na wanafunzi wengine wamewatambua wanafunzi waliotekwa. Hapo jana rais Muhammadu Buhari aliliamuru jeshi kuhakisha linawarudisha katika familia zao, wanafunzi wote waliotekwa.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments