Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wachezaji wa Namungo FC waliokwama Angola kutua leo bongo

 LEO Machi 2, wachezaji wa kikosi cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco wanatarajiwa kuwasili ardhi ya Bongo wakitokea nchini Angola.
Wachezaji hao wawili ni Lukas Kikoti na Hamis Fakhi ambao walianza safari jana kwa kupitia Ethiopia wakitokea Angola walikokuwa wameshikiriwa karantini kwa zaidi ya siku 16.

Walikwama wakati walipkwenda kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya 1 de Agosto pamoja na mwingine Fred Tangalo ambaye amebaki Angola.

Tangalo ambaye ni ingizo jipya kutoka ndani ya kikosi cha Lipuli amebaki Angola kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa majibu yake ya Corona bado hayajatoka.

 Namungo imetinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho na ipo kundi D.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments