Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Waliyomburuza na gari mama muuza ndimu wasimamishwa kazi Kenya

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREGavana wa kaunti ya Kisumu amewasimamisha kazi maafisa waliomburuza barabarani mwanamke mfanyabiashara wa matunda.Vyombo vya habari vimeripoti kuwa mwanamke huyo alikataa kutoa rushwa. Alikuwa akiuza machungwa na ndimu njia ya wapita kwa miguu eneo ambalo limepigwa marufuku kufanyika biashara.Mwanamke huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa mmoja kati ya maafisa hao alikaa kwenye gari aina ya pick-up akiwa amemshika mkono wake na kukataa kumuachilia wakati gari hiyo ilipokuwa ikiondoka.Dereva aliendesha chombo hicho cha moto mpaka katika kituo cha polisi cha karibu baada ya kundi la watu kuamua kukimbiza gari. Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya watu waliokuwa na ghadhabu waliokusanyika katika kituo hicho.

Gavana Anyang’Nyong’o amesema amewasimamisha kazi maafisa wote waliohusika na tukio hilo mpaka uchunguzi utakapokamilika.

Post a Comment

0 Comments