Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Wananchi Waonywa Kuchukua Mchanga Kaburi la Maalim Seif
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib ametoa onyo kwa watu wanaochukua mchanga wa kaburi la Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad kwani utaratibu huo haukubaliki.

 

Watu wanaokwenda kumuombea Dua Maalim Seif aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar wamekuwa na tabia ya kuchukua mchanga wa kaburi kwa madai unanukia Miski.RPC wa Kaskazini Pemba, Juma Sadi Khamis amesema watu wanaruhusiwa kwenda kumuombea dua marehemu lakini amewaonya kuchukua mchanga wa kaburi kwa sababu yoyote.

 

Maalim Seif Sharif Hamad ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, alifariki dunia Februari 17, 2021.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments