Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Wezi wapuliza dawa ya usingizi, wawaibia wafiwa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Pwani. Polisi mkoani Pwani wamekamata vifaa mbalimbali vilivyoibiwa katika msiba eneo la Mlandizi, Kibaha.


Akizungumza leo Alhamisi Machi 11, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema vifaa hivyo vimeibiwa baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wezi kufika  kwenye msiba wa mkazi mmoja wa Mlandizi  na kuwapulizia dawa ya usingizi baadhi ya waombolezaji na wafiwa.


“Watu walikuwa wamekwenda kuzika na wengi walitawanyika, wale wachache waliokuwa wamebaki   ilipofika usiku waliingia vyumbani kulala, hawa wezi walipulizia dawa ya usingizi na wafiwa walilala usingizi mzito ikawa rahisi kwao kuvunja kufuli, kuingia ndani na kuiba,” amesema


Ametaja baadhi ya vitu vilivyoibiwa ni televisheni na simu za mkononi  na kubainisha kuwa katika ufuatiliaji wa tukio hilo watuhumiwa kadhaa wamekamatwa wakiwa na simu mbili na televisheni hiyo, polisi bado wanaendelea kuwasaka wengine.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments