Ticker

6/recent/ticker-posts
.

2 wafariki, 2 wajeruhiwa kwenye ajali ya ndege iliyotokea nchini Mexico

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Wahudumu 2 kati ya 4 waliokuwa kwenye ndege wameripotiwa kupoteza maisha na 2 kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea nchini Mexico.
Ndege aina ya Cessna 206 iliyokuwa ikitoka kwenye kisiwa cha Holbox, karibu kilomita 65 kaskazini magharibi mwa Cancun, katika pwani ya Bahari ya Caribbean, ilifanya ajali na kuanguka baharini huko Cancun Lagoon.

Mmoja wa wahudumu wa ndege hiyo alifariki katika eneo la ajali wakati wa juhudi za uokoaji, na mwengine wa pili akafariki alipokuwa akifanyiwa huduma ya kwanza. Wahudumu wengine 2 walijeruhiwa.

Timu za ulinzi wa kitaifa, polisi na kikosi cha zimamoto zilishiriki katika juhudi za uokoaji.

Wakati hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa kuhusu chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo, uchunguzi umeanzishwa juu ya tukio hilo.

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments