Adaiwa kumuua mumewe siku 14 baada ya kufunga ndoa, kisa si chaguo lakeHappy Nyasumo (18) mkazi wa Wilaya ya Serengeti amemuua mumewe, Bebe Mbogo (26) kwa madai kuwa hampendi na hakuwa chaguo lake zikiwa zimepita  siku 14 tangu walipofunga ndoa.


Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Aprili 14, 2021 mkuu wa Wilaya ya Serengeti,  Nurdin Babu amesema tukio hilo limetokea jana Aprili 14, 2021 saa 4 usiku katika kitongoji cha Pengo kijiji cha Iseresere.Amesema chanzo ni mgogoro wa ndoa na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa hatua zaidi.Diwani wa Majimoto,  Johannes Masirori ambaye ni mjomba wa marehemu amesema Mbogo na Happy walifunga ndoa Machi 31, 2021 na kudai kuwa mwanamke huyo amekiri kufanya mauaji hayo."Kabla ya mauaji anadai kuwa mumewe alimlazimisha kufanya tendo la ndoa na baada ya kumaliza mwanaume alilala na yeye alipobaini amesinzia akachukua panga  na kumkata mara tatu shingoni,” amesema.Amesema baada ya kufanya kitendo hicho Happy alikwenda kwenye nyumba ya mkwewe na kuchukua chakula na kuanza kula."Ameulizwa na kusema bila hofu na kuwaonyesha panga alilokuwa ameficha..., tangu wamefunga ndoa wamekuwa katika mgogoro mkubwa. Happy alirudi kwao kwa madai kuwa hamtaki mumewe lakini huko kwao wakamlazimisha arudi kwa mumewe kwa maelezo kuwa hawawezi kurudisha ng'ombe waliochukua wakati wakimuozesha," amesema.Masirori amesema wakati watu wakilia na kusikitika kutokana na tukio hilo, mtuhumiwa hakuwa na wasiwasi na aliwataka wasiojua wamtazame vizuri.


đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad