google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Afrika inahitaji ujuzi kutengeneza chanjo yake yenyewe – Rais Ramaphosa | UDAKU SPECIAL

Afrika inahitaji ujuzi kutengeneza chanjo yake yenyewe – Rais Ramaphosa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema Afrika inahitaji ujuzi na uwezo wa kutengeneza chanjo yake.


Kwenye mkutano wa viongozi wa Kiafrika, alisema ulimwengu ulikuwa ukishuhudia “chanjo ya ubaguzi wa rangi”.

Na ni ukweli kwamba kati ya mamia ya mamilioni ya chanjo ambazo hadi sasa zimetolewa, chini ya 2% zimewafikia Waafrika.

Mpaka sasa Afrika ina idadi ndogo ya maambukizi ya Covid-19 ikilinganishwa na Ulaya na Marekani.

Hii imeelezwa kuwa ni kwasababu serikali nyingi za Afrika zilichukua hatua haraka ya kufunga mipaka na kuweka vizuizi.

Lakini Shirika la Afya duniani limetahadharisha kuwa wimbi jingine la maambukizi huenda likarejea na kuwa nchi zilizo na mifumo duni ya afya zinaweza kuathirika.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad