Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Aliyefukuzwa Kazi Kwa Kurekodi Ndege ya China Ikitua Kenya Arudishwa Kazini

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREMfanyakazi wa Shirika la Ndege la Kenya, Ali Gire kurejea kazini baada ya shirika hilo kufuta barua ya kumtimua kwa kurekodi video ya ndege ikitua Nairobi ikiwa na abiria 239 ikitoka China

Haya yamebainika leo katika Mahakama moja Jijini Nairobi ambapo Maafisa wa Shirika hilo (KQ) wamemthibitishia Jaji Weldon Korir kwamba hatashtakiwa

Alikuwa ametimuliwa kwa kurekodi video ya ndege ya China Southern Airlines ikitua katika Uwanja wa Jomo Kenyatta ikitokea China ambapo ndio chimbuko la #coronavirus

Mahakama Kuu tayari ilikuwa imezuia Ali ambaye ni Afisa wa usalama katika Uwanja wa Kimaifa wa Jomo Kenyatta, kukamatwa au kufunguliwa mashtaka

Haya yanajiri siku moja baada ya Waziri wa Uchukuzi, James Macharia kuwaambia Wabunge kwamba Ali ni mtu aliyetekeleza uhalifu anayefaa kukumbana na mkono wa sheria

Post a Comment

0 Comments