Baba agomea msiba wa mtoto wake, arudishiwe uhai

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 



Baba mzazi wa kijana Kusekwa George mkazi wa mtaa wa Ihushi kata ya Kishiri, Nyamagana Mwanza, amekataa kuhudhuria msiba na shughuli ya kuaga mwili wa mwanaye huyo mwenye miaka 17.

 

Mzee George amekataa akishinikiza mwili wa kijana huyo anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa na Mwenyekiti wa mtaa pamoja na Sungusungu, upelekwe kwa Mwenyekiti kisha amrejeshe mwanaye akiwa hai.


Kwa upande wa wakazi wa mtaa wa Ihushi kata ya kishiri wilayani Nyamagana mkoani Mwanza wamesema hawatauzika mwili wa kijana Kusekwa George.


 


Wananchi wamedai kuwa kijana huyo aliuawa kwa kupigwa na marungu, fimbo pamoja na mkanda wa mashine na mwenyekiti wa mtaa akishirikiana na Sungusungu.


Wananchi hao leo Aprili 8, 2021, wameupeleka mwili wa kijana Kusekwa nyumbani  kwa Mwenyekiti huyo ili amrudishie uhai wake.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad