Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Baba Levo Alimwa Faini Mil 1 Basata, Naye Ataka Mil 6 kwa Harmonize

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limempiga faini ya Tsh milioni moja msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo kwa kusambaza wimbo bila kuupeleka kuhakikiwa na Baraza hilo kwa mujibu wa kanuni.

 

Msanii huyo ameeleza hayo leo Ijumaa Aprili 16, 2021 ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia sababu ya kuitwa Basata na polisi jana.

 

“Kwa Basata nilikwenda kwa sababu ya huo wimbo ambao niliuachia bila kuhakikiwa na leo nimepokea barua ya kutozwa faini.

 

“Kubwa ni kuhusu wimbo wangu wa Harmo…. ambao haukupitia taratibu katika kuutoa na tayari nimepokea barua ya onyo na kupigwa faini,” amesema Baba Levo.

 

Aidha, Baba Levo amesema atakwenda mahakamani kudai fidia ya Tsh milioni sita kwa kuzushiwa kuwa amesambaza picha za utupu za Harmonize.

 

 

Kuhusu kwenda polisi, msanii huyo amesema ni madai kuwa amesambaza picha za utupu za msanii Harmonize na kueleza kuwa anasubiri kesi hiyo ifike mahakamani ili adai fidia ya Sh6 bilioni kwa kuwa anaamini hajahusika.

 

 

“Mimi ni brand kubwa naaminika na watu sasa leo unanichafua kwa vitu vya uongo, sitakubali nangoja tufikishane mahakamani ili nidai fidia yangu,” amesema.


 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments