Bado hatujakata tamaa, Tutazidi kupambana - Uongozi wa Yanga

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa licha ya kupoteza mchezo wao jana mbele ya Azam FC bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zijazo na hawajakata tamaa.

Uwanja wa Mkapa, saa 2:15 usiku, kulikuwa na mpambano mkali kwenye mchezo wa ligi ambapo Azam FC ilishinda bao 1-0.

Ni Prince Dube ambaye alipachika bao pekee la ushindi dakika ya 85 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango, Faroukh Shikalo na kuwafanya wapoteze mchezo huo wa mzunguko wa pili.

Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga amesema kuwa ni matokeo mabaya ambayo wanayapata watayafanyia kazi.

"Hakuna kukata tamaa. Tuendelee kupambana kwenye kila mchezo kwa kila namna ibakie matokeo ya mpira na bahati ya siku yenyewe." 

Azam FC inafikisha jumla ya pointi 54 ikiwa nafasi ya tatu huku Yanga ikibaki kuwa na pointi 57 nafasi ya pili kwenye msimamo. Kinara ni Simba mwenye pointi 58 baada ya kucheza mechi 24.Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad