Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Bongo Flava Tunaonekana Hatuna Adabu Kwa Hili la Paula, Tumuheshimu Basi Hata P Funk

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BUREJamani eeeh.... Kama mmechagua Kumchukulia poa Kajala sawa mumemzoea sijui, ila mimi binafsi namheshimu Lakini Yote Mnayofanya Kabla na baada Ya kuyafanya Kumbukeni kuna huyu mtu muhimu sana na mzito kwenye Game hii ya BongoFlava
Mtu huyo ni Legendary mwenye heshima juzi jana leo na kesho....

“Producer P Funk Majani” bila juhudi za kichwa na mkono wake na mikono ya ma producer wengine wachache basi leo hii Tusingekua tuna enjoy Muziki huu wa BongoFlava wa leo ambao unawapa maisha vijana wengi maelfu kwa maelfu nikiwemo mimi #MbeaWaKimataifa
“Asiekumbuka historia yake ni mtumwa”

Kina PFunk Walianza kuuzalisha Muziki Huu angali ukiwa mchanga kabisaaaaa kabla ya kuwa biashara mpaka leo muziki huu umekua biashara”
Kumhusisha mtoto wake kwenye haya mambo ni kumvunjia heshima mbele ya macho yake, tena cha kushangaza wanaomhusisha Paula kwenye haya mambo ni Wasanii wa muziki huu huu wa BongoFlava”

Wakati wao wanafungua njia kwa ajili ya kizazi kipya cha BongoFlava walifanya kwa nia njema ya kukuza game, laiti wangejua kingekuja kutokea nini leo hii Dah.... ingewavunja moyo mapemaaa... maana yake leo hii tungekua tunacheza makirikiri ya nchi nyingine za afrika.
Sio sifa kupigana vita katikati ya mtoto wa PFunk

Nawausia ndugu zangu maelfu kwa maelfu Tunao neemeka na BongoFlava
Tunajishusha hadhi kwa kuonekana Hatuna Adabu, mbele ya Producer PFunk Na Mbele ya Serikali na mbele ya jamii ya kimataifa na mbele ya watanzania kwa ujumla

Wote Walioshiriki Kwenye Hili Jambo tangu story inaanza mpaka leo wanapaswa kumwomba radhi Legend @majani187 na kutubu kwa mola wao, kwani hizi sio sifa nzuri

Kwa kuanza mimi naanza na kuwaombea Radhi “Legendary PFunk Majani naomba uWasamehe mapaka shume hawajui walitendalo” 🙏

Post a Comment

0 Comments