Brian Simba Afungasha Virago Lebo ya Vanessa Mdee

 


Rapa aliyekuwa anamilikiwa na rekodi lebo ya Mdee Music chini ya msanii Vanessa Mdee aitwaye Brian Simba, amesema amemaliza mkataba wa kusimamiwa na lebo hiyo na hivi sasa yupo huru kufanya kazi zake mwenyewe.


Brian Simba amesema anamshukuru sana Vanessa Mdee kufanya nae kazo kwani amempa uzoefu mpya kwenye upande wa muziki pia amemfanya kuzunguka mikoa na nchi mbalimbali.


"Masomo hayajanirudisha nyuma yamenipa 'exposure' mpya kwenye maisha, kufanya kazi na Vanessa Mdee ilinisaidia vitu vingi kama kuzunguka mikoa na nchi mbalimbali, ilikuwa experience nzuri ila mkataba wetu wa kufanya kazi uliisha" amesema Brian Simba 


Pia amezungumzia kuhusu ujio wa Album yake mpya na uwepo wa wasanii wengine wapya wanaofanya muziki wa HipHop  kwa kusema  "Album yangu itatoka mwezi wa nane ina ngoma nyingi sana na kali, hapo katikati nilipokuwa shule walikuja marapa wengi wakali ila ni marafiki zangu wote, napenda wakali tuwe wengi".


đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đŸ’¥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đŸ’¥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad