Bwalya: Tutafanya Maajabu Kimataifa… Droo Ya CAF Leo
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Larry Bwalya amesema kuwa timu hiyo ina nafasi kubwa ya kufanya maajabu katika Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo inatarajiwa kupangwa leo Ijumaa.

 

Bwalya alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu baada ya kiwango chake kufurahishwa na mabosi wa timu hiyo.

 

Akizungumza na Championi Ijumaakuelekea kwa droo hiyo ambapo Simba ndiyo itajua mpinzani wake, Bwalya alisema: “Imekuwa heshima kwangu na timu pia kuona tunafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika michuano ya kimataifa.“Kwa sasa tunasubiri ratiba na timu ambayo tutacheza nayo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

“Bado tunayo nafasi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kutokana na maandalizi mbalimbali ambayo tunaendelea kufanya, “ alisema Bwalya.

 

Katika droo ya leo Simba inatarajiwa kupangwa na wapinzani kati ya hawa, CR Belouizdad au MC Alger zote za Algeria au Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini

Stori: Leen Essau,Dar es Salaam


💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad