CAG: Stendi ya Magufuli Itasababisha Foleni Morogoro Road

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imesema ujenzi wa kituo cha mabasi cha Magufuli kilichopo Mbezi mkoani Dar es Salaam haukujumuishwa katika upanuzi wa barabara kutoka Kimara kwenda Kibaha mkoani Pwani.
 

Ripoti hiyo ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 imesema kujengwa kwa kituo hicho ambacho kimeanza kutumika kutaleta msongamano katika makutano ya barabara.
 

“Kulingana na mahojiano na maafisa wa Wakala wa Barabara (Tanroads) na jinsi tulivyoona kwenye eneo la mradi, nilibaini kuwa mradi wa upanuzi barabara ya Morogoro haupo kwenye mwelekeo wa kufikia malengo yake ya kupunguza msongamano wa vyombo vya usafiri kutokana na ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mbezi Mwisho.”



“Ujenzi huu ulianzishwa wakati mradi wa upanuzi unaendelea. Kwa hivyo, kituo cha mabasi hakikujumuishwa katika mpango na usanifu wa mradi huu. Zaidi ya hayo, uendeshaji wa kituo cha mabasi mbali na kusababisha msongamano wa magari unaweza kusababisha changamoto zaidi kwenye makutano yanayoingia barabara ya Morogoro. Kituo hiki cha mabasi kinatarajiwa kuhudumia mabasi 700 kila siku,” amesema.



Ripoti hiyo imesema wakati Tanroads inaandaa mikakati ya upanuzi wa barabara ya Morogoro, Wizara ya Tamisemi kupitia Jiji la Dar es Salaam, walikuwa wakipanga mikakati ya ujenzi wa kituo hicho.

 

“Mipango hii miwili ilifanywa bila ushirikiano kati ya taasisi hizi za serikali. Ukosefu wa mpango mkuu jumuishi wa kisekta baina ya taasisi za umma ndio chanzo kikuu cha tatizo hili,” amesema CAG.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad