Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Camera ya Mwilini ya Polisi Yaonesha Derek Chauvin Akimkaba Shingo George Floy

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Askari Derek Chauvin yupo kizimbani ikiwa leo ni siku ya tatu ya kusikilizwa kwa kesi hiyo ya mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd. Sasa camera ya mwilini (bodycam) iliyokuwa kwenye nguo za Derek Chauvin imeachiwa hadharani na inamuonesha akimkaba shingo kwa mikono kabla ya kumuangusha chini.


Jopo la majaji limeoneshwa video hiyo ambayo inamuonesha George Floyd akimuomba Chauvin amuachie kwa sababu yeye sio mtu mbaya kabla ya kumuangusha chini na kumkanyaga shingoni kwa zaidi ya dakika 9 hadi Kufa.


Katika harakati za kumkamata George Floyd, Derek Chauvin akiwa na mwenzake Thomas Lane ambapo camera hiyo iliwaonesha wakitumia nguvu kumuingiza kwenye gari ya polisi na baadaye camera hiyo ilidondoka chini.


Camera ya shuhuda Charles McMillan ndiyo ilionesha tukio zima la Chauvin kumkandamiza na goti George Floyd hadi kufa. Kuna muda McMillan alisikika akimwambia Floyd akubali tu kushirikiana na askari kwani hawezi kushinda.


Wakati akitoa ushahidi wake, McMillan mwenye umri wa miaka 61 aliangua kilio kwa dakika 10 wakati camera ile ikionesha tukio zima la mauaji ya George Floyd mnamo Mei 25, 200. McMillan alisikika akimwambia Chauvin, "Ondoa goti lako kwenye shingo yake."

-

Shuhuda mwingine wa tatu kwenye kesi hii Donald Williams alisikika akimwambia Chauvin siku hiyo ya mauaji kwamba "Huyu jamaa atakuandama maisha yako yote."

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments