Ticker

6/recent/ticker-posts
.

DMX mahututi hospitali Marekani

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Rapa DMX wa Marekani yuko hali mahututi hospitalini baada ya kupata mshtuko wa moyo, amesema wakili wake Murray Richman.Bwana Richman ameviambia vyombo vya habari vya Marekani hana ufahamu ikiwa chanzo cha mshtuko huo wa moyo ni utumiaji wa dawa za kulevya kupita kiasi, kama ilivyoripotiwa na TMZ.

DMX amekuwa akikabiliana na matumizi ya dawa za kulevya kwa miaka mingi tu taarifa ambazo zimekuwa zikijulikana na umma, pia amekuwa katika kituo cha kurekebisha tabia mara kadhaa.

Rapa huyo anachukuliwa kama nyota wa muziki wa hip-hop, na ameshirikiana na wasanii kadhaa kama vile JAY-Z, Ja Rule, Eve na LL Cool J pamoja na kushiriki filamu kadhaa.

Mwanamuziki huyo, 50, ambaye jina lake kamili ni Earl Simmons, alipelekwa hospitali huko White Plains, New York Ijumaa jioni, Bwana Richman amesema, akiwa na familia yake.

“Alikuwa akipumua kwa mashine,” wakili huyo amesema. “lakini sasa hivi hatumii tena mashine. Anapumua mwenyewe ila utendaji wa ubongo ni mdogo mno.”

Aidha mwanamuziki huyo, amewahi kufungwa jela miaka ya nyuma kwa makosa ya ukatili dhidi ya wanyama, uendeshaji mbaya wa gari, umiliki wa dawa za kulevya na silaha kinyume cha sheria.

Mwaka 2018, aligonga vichwa cya habari kwa kumchezea jaji mmoja nyimbo yake alipokuwa anakabiliwa na makosa ya kukwepa kulipa kodi. Baada ya kusikiliza nyimbo hiyo, jaji aisema DMX ni “mtu mzuri” na kutoa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja gerezani dhidi ya mwanamuziki huyo.

Mwaka 2016, alipata matatizo ya kupumua kabisa na ikabidi apate huduma za kumfufua kwa mashine haraka sana katika hoteli moja mjini New York.

DMX amekuwa katika taaluma yake kwa miaka 20, pamoja na muziki, ameshiriki filamu kadhaa zikiwemo za ‘Cradle 2 the Grave na Romeo Must Die’, zote mhusika mkuu akiwa ni Jet Li.

“Earl ni mtu mzuri,” Bwana Richman amesema. “Earl ni mtu ambaye angeweza kukuelezea simulizi. Inavunja moyo sana.”

Post a Comment

0 Comments