Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

DR. BASHIRU: ALIYE NA DOLA ANANUFAIKA NA DOLA HIYO KUBAKI MADARAKANIKatibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amesema "Ni vizuri vyama vya siasa vinavyotamani kuingia madarakani vijue kwamba chama kilichopo madarakani kinatumia mchango na nguvu za ziada"

Akiwa kwenye mazungumzo na Waandishi wa Habari wa IPP amesema "Aliye na Dola ananufaika na Dola hiyo kubaki madarakani, huo ni ukweli. Hata CHADEMA ikiingia kwenye Dola kuiondoa kwenye Dola utakuwa ni uzembe wake."

Amesisitiza wanaosubiri wawe (CCM) legelege katika kutumia Dola kubaki kwenye Dola watasubiri sana kwani kuna faida kubwa chama kilichopo madarakani kutumia Dola kufanya mambo ya kujenga imani kwa wapiga kura ili kibaki madarakani

Lakini pia amebainisha kuwa CCM imejiandaa kushinda kihalali, na ushindi wenyewe sio wa Oktoba, bali ulianza kutafutwa tangu mwaka 2015

Ameongeza "Ninachoomba mimi Wanasiasa wenzangu wafuate sheria, maelekezo na taratibu kwa sababu nchi hii tukigeuza kuwa wakati wote ni kusema chochote na kufanya chochote, tutatafutana. Ni vizuri tukajenga nidhamu"

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments