Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Fahamu kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhan na yasiostahili kufanywa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE
Mwezi wa Ramadhani ni mwezi mtukufu zaidi kwenye kalenda ya mwaka wa kiislamu.

ramadan, ramadan 2021, ramadan moon sighting, ramadan 2021 moon sighting, ramadan 2021 moon sighting today, ramadan moon sighting 2021, moon sighting india, moon sighting today india, ramadan moon sighting in india, ramadan moon sighting today time, ramadan moon sighting today time in india, ramadan moon sighting time, moon sighting today saudi, moon sighting saudi, ramadan moon sighting in pakistan, ramadan moon sighting in india, ramadan moon sighting in uae, ramadan moon sighting saudu arabia, ramadan ka chand, ramadan ka chand time

Ni mwezi pia unaofahamika kama mwezi wa toba, kipindi ambacho waumini wa dini hiyo wanajisogeza karibu zaidi na Mola wao kwa ibada mbalimbali ili wavune thawabu.

Ni dhahiri pia kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kunakuwa na mabadiliko mengi katika mfumo wa maisha na matendo ya watu.

Katika nchi ambazo raia wake ni wa dini mbalimbali kama Afrika Mashariki, maswali mengi huibuka kipindi hiki juu ya nini kinatakiwa kifanyike ama kisifanyike.

Wale ambao si waislamu huwa na maswali mengi juu ya nini wanaweza kufanya ama kutofanya mbele ya ndugu, jamaa au marafiki wa kiislamu.

Lakini hata kwa baadhi ya waislamu huwa wanatatizika juu ya maswali kama hayo.

Haya ni baadhi ya maswali hayo makuu:

Je, naweza kula mbele yako?
Tendo kubwa ambalo linaonekana moja kwa moja kufanywa na waislamu katika kipindi hiki cha mfungo ni kujizuia kunywa na kula kutoka alfajiri (kuchomoza kwa jua) mpaka magharibi (kuzama kwa jua).

Haijalishi, mtu awe masikini ama tajiri, awe na chakula ndani ama asiwenacho, madhali wanakiri kwa yakini kuwa ni waislamu basi hujizuia kula na kunywa.

Katika mazingira yenye watu wa imani tofauti, mathalani mtaani, shuleni au hata kazini sio wote wanaofunga, na wengine hutembea na vyakula vyao.

Swali huwa, je, naweza kula mbele yako?Futari

Jibu lake hutegemeana na mtu na mazingira husika. Kuna wale ambao hawana tatizo lolote kwa mtu kula mbele yake anapokuwa amefunga, ila wengine wanatafsiri ukifanya kitendo hicho kama kutowaheshimu na kuwapa majaribio ya kiimani kwa makusudi.

Kama upo kazini ama shuleni, ni vyema zaidi ukatumia maeneo maalumu yaliyotengwa kwa chakula.

Mazingira ya eneo pia huchangia katika hili. Katika nchi nyingi ambazo zinafuata sheria za kiislamu, kula hadharani wakati wa mchana wa mwezi wa Ramadhani huwa ni kosa. Na ukifanya hivyo unaweza kujipata mikononi mwa vyombo vya usalama.

Hata katika baadhi ya nchi ambazo hazifuati sheria za kiislamu, lakini kuna Miji ambayo waislamu ni wengi zaidi, mathalani ukanda wa pwani wa Afrika Mashariki, ni kinyume cha maadili kula hadharani pia. Zipo baadhi ya sehemu kama visiwani Zanzibar ambapo hupitisha katazo rasmi la watu kufanya hivyo.

Kwa mtu aliyefunga, kunywa ama kula kabla ya magharibi huvunja funga yake moja kwa moja.

Tendo la ndoa
Katika sheria za kiislamu, tendo la ndoa ama ‘jimai’ limehalalishwa kwa wanandoa tu (mke na mume) na si kinyume cha hapo.

Hivyo, hakuna swali juu ya watu wanaoishi bila ndoa wakati wa Ramadhani kama wanafunga ama la. Kwa wao kuishi pamoja bila ndoa tu kwa imani ya dini hiyo ni dhambi kubwa, na ikiwakutia ramadhani wanahesabika hawajafunga hata kama watajizuia kula na kunywa kwa mwezi mzima huku wakiishi pamoja.

Lakini hata kwa wanandoa, tendo la kujamiiana halitakiwi kufanyika wakati wakiwa ndani ya saumu (wakati wote baina ya alfajiri na magharibi). Endapo watafanya hivyo ndani ya muda wa kufunga basi funga yao itakuwa imebatilika.

Lakini baada ya jua kuzama, wanandoa wanaruhusiwa kujamiiana.

“Mmehalalishiwa usiku wa saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni nguo kwenu na nyinyi ni nguo kwao. Mwenyezi Mungu anajua mlikuwa mkizikhini nafsi zenu … Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyokuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku…” imeelekeza Kurani sura ya 2 aya ya 187.

Vipi kuhusu kupeana mkono na kukumbatiana?Elevated View Of A Male Manager Shaking Hands With Female Applicant At Workplace
Hakuna shida yoyote kwa mwanaume wa kiislamu aliyefunga kupeana mkono ama kukumbatiana na mwanaume asiye wa kiislamu ambaye hajafunga katika mwezi huu.

Pia hakuna shida yoyote kwa mwanamke wa kiislamu na mwanamke asiyekuwa muislamu kufanya hivyo.

Shida inakuja kwa mwanamke na mwanaume wawe wa kiislamu wote, ama muislamu na asiyekuwa muislamu kupeana mikono na kukumbatiana.

Katika jambo hilo hata nje ya mwezi wa ramadhani wasomi wa kiislamu wametofautiana. Kuna wale wanaoamini kuwa hakuna shida yeyote kwa wanaume na wanawake ambao si ndugu wa damu kupeana mikono alimradi haiamshi hisia za matamanio.

Lakini kuna wale ambao wanaamini kupeana mikono na kukumbatiana ni jambo lisilostahili, na endapo litafanyika mwezi wa ramadhani basi litapunguza nguvu ya funga ya mhusika japo saumu yake haitabatilika.

Hivyo, usije ukashangaa rafiki yako muislamu wa jinsia tofauti ambaye ulikuwa umezoea akikupa mkono wakati mkisalimiana awali, akiepuka mkono wako katika mwezi huu.

Kusema uongoWaumini wakisali
Kusema uongo ni jambo baya kwenye uislamu. Imepokelewa kuwa Mtume Muhammad amesema kuwa “(kusema) uongo ni haramu, hata kama ni mzaha.”

Pia moja katika alama tatu za mtu mnafiki kwa mujibu wa mtume huyo ni mtu kusema uongo.

Vipi kuhusu uongo kwenye saumu? Kauli maarufu ya mtume juu ya hilo inasema: “Yeyote ambaye hawezi kuacha maneno ya uongo na kuufanyia kazi uzushi, basi Mwenyezi Mungu hana haja naye yeyote ya kuacha chakula chake na maji yake.”

Wasomi wa kiislamu wanatafsiri kauli hiyo kuwa uongo na uzushi haubatilishi saumu bali unapunguza thamani ya funga ya mtu.

Lengo la waislamu kufunga ni kuwa Wacha Mungu, na uongo si sifa ya Ucha Mungu.

Post a Comment

0 Comments