Ticker

6/recent/ticker-posts
.

FIFA Yaifungia Chad Kimataifa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

Shirikisho la soka duniani, FIFA limeifungia Chad katika mashindano ya dunia ya kandanda baada ya serikali ya nchi hiyo iingilie kati namna ambavyo shirikisho la soka nchini humo inavyofanya kazi.

 

 

Hatua hii imekuja baada ya waziri wa vijana na michezo kuvunja shirikisho la soka nchini Chad mnamo mwezi Machi.

 

 

Baada ya tangazo hilo lililotolewa na serikali ya Chad , shirikisho la soka barani Afrika liliitoa timu ya taifa katika raundi ya pili ya kufuzu kuingia kombe la mataifa ya Afrika.

 

 

Chad haipo kwenye michuano yeyote ya kimataifa baada ya kuondolewa katika mashindano ya kombe la dunia ya mwaka 2022 na Sudan mwaka 2019.

 

 

Taarifa rasmi kutoka shirikisho la soka la dunia limesema: “baraza la Fifa linaweza kuondoa marufuku hayo muda wowote kabla ya mkutano ujao wa Fifa na tutatoa taarifa rasmi.” Mkutano ujao unatarajiwa kufanyika mtandaoni Mei 21.


 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments