google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Gomes Ahamishia Hasira Zake Yanga | UDAKU SPECIAL

Gomes Ahamishia Hasira Zake Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




LICHA ya kwamba jana alikuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya AS Vita kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, lakini hasira za Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes zipo ndani ya Ligi Kuu Bara kuhakikisha anaishusha Yanga kileleni.

 

Gomes ambaye msimu huu ana kibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara, Mei 8, mwaka huu atakutana na Yanga kwa mara ya kwanza tangu awe kocha wa Simba.

 

Kabla ya timu hizo kukutana, Simba itacheza mechi tano za ligi ambazo ni sawa na dakika 450, huku Yanga iliyo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi, ikiwa na dakika 360, sawa na mechi nne.



Mechi za Gomes ni dhidi ya Mtibwa Sugar (Aprili 14), Mwadui FC (Aprili 18), Kagera Sugar (Aprili 21), Gwambina (Aprili 24) na Dodoma Jiji (Aprili 27), kisha ndiyo anakutana na Yanga.

 

Kwa upande wa Mwambusi, yeye atakuwa na kazi mbele ya KMC (Aprili 10), Biashara United (Aprili 17), Gwambina (Aprili 20), Azam (Aprili 25), kisha atapambana na Simba ya Gomes.

 

Gomes raia wa Ufaransa, ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Mechi zote kwetu ni muhimu kupata pointi tatu, kwani ukitazama tunahitaji kuongoza ligi ili kufi kia lengo la kutwaa kombe, haitakuwa kazi rahisi, nimewaambia wachezaji wana kazi kubwa ya kufanya.

 

”Msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa sasa unaonesha Yanga inaongoza ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 23, huku Simba ikiwa ya pili ikikusanya pointi 46 ikishuka dimbani mara 20.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad