Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Grealish awaliza mashabiki wa Aston Villa

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

 


Kocha wa klabu ya Aston Villa, Dean Smith amethibitisha kuwa nahodha na kiungo wake tegemezi Jack Grealish ataendelea kuwa nje ya uwanja wa zaidi ya wiki mbili baada ya kupata maumivu mengine ya nyama za paja akiwa kwenye harakati za kujiuguza na kupona kurejea uwanjani.

 


Smith amesema “Mimi na Jack tuliamini atarejea hivi karibuni lakini amepata maumivu ya nyama za paja ambayo yatamfanya azidi kuwa nje ya wiki kwa wiki mbili”.


“Alikuwa vizuri sana mazoezini, lakini hakuweza kuvumilia na kuendelea. Ni majeraha ambayo yanamhitaji apate nafasi ili arejee”.


Taarifa hiyo itawapa simanzi mashabiki wa Aston Villa kwani nahodha huyo amefunga mabao muhimu 6 na kutengeneza mengine 12 na kuisaidia Villa kushika nafasi ya 9 wakiwa na alama 44 baada ya michezo 29.

Post a Comment

0 Comments