Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Harry Kane atoa neno la shukrani kwa Jose Mourinho


Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane amesema ilikuwa ni furaha kubwa kwake kufanya kazi na kocha Jose Mourinho.
Mourinho alitimuliwa kwenye timu hiyo baada ya kupata matokeo mabaya kwenye michezo yake sita mfululizo ya hivi karibuni. Kane kwa sasa ni kinara wa mabao kwenye timu hiyo amesema Mourinho alikuwa mtu safi sana kwenye timu hiyo.

“Nakushukuru sana bosi kwa kila kitu, ilikuwa jambo zuri sana kuona kuwa tumefanya kazi pamoja.

“Hakika ulikuwa mtu muhimu kwetu nakutakia kila la kheri kwenye majukumu yako yajayo” aliandika Kane mshambuliaji mahiri wa timu ya Taifa ya England.

Mourinho ametimuliwa siku chache kabla Spurs hawajacheza fainali ya Kombe la Carabao, dhidi ya Man City Jumapili ijayo na atalipwa pauni milioni 28, sawa na shilingi bilioni 69.

Timu hiyo msimu huu imeshindwa kufanya mambo makubwa kwenye ligi ikiwa sasa inashika nafasi ya saba na pointi 50, imeshinda michezo 14 na kupoteza michezo kumi baada ya kucheza michezo 32.

Mbali na Kane, pia staa wa Spurs, Son Heung-min, amesema kuwa anamshukuru sana Mourinho kwa juhudi zote alizofanya kwenye timu hiyo.


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments