Hii ndio picha pendwa ya Malkia wa Uingereza Elizabeth akiwa na marehemu mume wake Prince Philip




Malkia Elizabeth ameitoa kwa umma moja ya picha zake anazozipenda sana akiwa pamoja na mume wake wa miaka 73 , Mtawala wa Edinburgh, katika siku ya mazishi yake.



Wanandoa hao wa ufalme wa Uingereza walipigwa picha hiyo wakiwa wamepumzika kwenye majani katika eneo zuri la Aberdeenshire katika picha iliyochukuliwa na mkuu wa kaunti ya Wessex mwaka 2003.

Philip anaonekana akiwa amelala nyuma, huku akiwa ameegemea kiwiko, huku kofia yake ikiwa imetundikwa kwenye goti lake.

Mazishi yake yalifanyika katika kasri la kifalme la Windsor Castle saa tisa kwa saa za Uingereza(15:00 BST) Jumamosi.

Watoto wa Mtawala huyo walitembea nyuma ya jeneza lake wakati wa matembezi ya kuusindikiza mwili wake.

 

Katika picha hiyo iliyopigwa katika siku iliyokuwa ya jua karibu na mji wa Aberdeenshire wa Ballater, Malkia na Mwanamfalme Philip walionekana watulivu na walimtazama kwa tabasamu mkwe wao Sophie ambaye alipiga picha hiyo.

Malkia – alikua amevalia sketi, blauzi na sweta pamoja na shanga shingoni-huku wakiwa wameketi na mume wake.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad