Ticker

6/recent/ticker-posts
.

Israel imesema imeidungua ndege isiyo na rubani kutoka Lebanon

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE


Jeshi la Israel limesema imeidungua ndege inayorushwa bila ya rubani ambayo iliingia katika anga yake kutoka Lebanon na kuonesha nyingine kama hiyo ambayo ilidunguliwa hapo awali. 
Taarifa ya Jehi la Isreal IDF imesema imeitambua ndege hiyo kuwa inalihusu kundi la Hezbollah ambalo linaungwa mkono na serikali ya Iran. 

Hata hivyo hakujawa na taarifa yoyote kutoka Lebanon au hata Hezbollah. 

Kimsingi Israel na Lebanon zinaonekana kama bado zipo katika vita, na Jeshi la Umoja wa Mataifa linaendelea na jukumu la kiusalama kwa kupiga doria zake katika mipaka ya matiafa hayo mawili. 

Mapema Feburuari, Hezbollah ilisema imeidungua ndege isio na rubani ya Israel, katika tukio ambalo Israel ilisema ndege isiyo ya kivita imepata ajali.

Post a Comment

0 Comments